Tuzo hiyo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, na kupokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha John Mshomba wakati wa ufungaji wa maonesho hayo.
Aidha, NSSF imeshinda tuzo ya mshindi wa kwanza katika kundi la Hifadhi ya Jamii na Huduma za Bima zilizotolewa Oktoba 12, 2024 na Mhe. Anthony Mavunde, Waziri wa Madini, wakati wa maonesho hayo.
kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa NSSF Bw. Mshomba amesema utoaji wa huduma kidijitali umekuwa nyenzo muhimu katika kuhakikisha huduma za NSSF zinawafikia wanachama popote walipo, ikiwemo kufungua madai ya kuomba mafao mbalimbali na kuwataka waajiri wa sekta binafsi kuhakikisha wanasajili wafanyakazi wao NSSF.
Naye, Bw. Omary Mziya, Mkurugenzi wa Uendeshaji, amesema Mfuko utaendelea kutoa huduma bora kwa wanachama kupitia mifumo ya TEHAMA ambapo hivi sasa wanachama wanaweza kufungua madai yao kwa njia ya kidijitali bila ya kulazimika kufika katika ofisi za NSSF.
Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Bi. Lulu Mengele ameeleza kuwa kupitia maonesho hayo Mfuko ulifikisha elimu ya hifadhi ya jamii kwa makundi mbalimbali yakiwemo ya wachimbaji wadogo wa madini pamoja na wajasiriamali zaidi 1500 Wilayani Bukombe.
"Maonesho ya madini yalikuwa fursa kwa NSSF kufikisha elimu ya hifadhi ya jamii, kuandikisha wanachama wapya kutoka sekta isiyo rasmi, tutoa elimu kuhusu huduma za kidijitali pamoja na fursa za nyumba na viwanja" amesema Bi. Lulu.
Awali, Meneja wa NSSF Mkoa wa Geita, Bi. Winniel Lusingu amesema katika mwaka wa fedha 2024/25, Ofisi ya Mkoa huo imeweka lengo la kukusanya shilingi bilioni 104 na kuwa mwaka wa fedha uliomalizika walikusanya shilingi bilioni 64.
Mwandishi; Ellukagha Kysa
Muhariri; Ramadhan Zaidy
0 Comments