Wadau wa maendeleo katika sekta ya afya wameahidi kuendelea kuchangia sekta ya hiyo wakati wa utekelezaji wa Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote.
Akizungumza katika kikao kilicho wakutanisha wadau wanaoshirikiana na Serikali kupitia sekta ya afya Oktoba, 21 jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu amewahimiza wadau kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali wakati wa kutekeleza Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote.
“Kwakuwa mpango huu unalenga kuendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za afya nchini, nitoe rai kwa wadau wote kuunga mkono juhudi za Serikali kuhakikisha tunatekeleza mpango huu wa kihistoria kwa nchi yetu,” amesema Dkt. Jingu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wadau wa maendeleo wanaoshirikiana na Serikali kupitia sekta ya Afya ambaye pia ni Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia ofisi ya Tanzania Dkt. Mustafa Abdalla, amesema kuwa wadau wako tayari kuendelea kutoa ushirikiano kwenye maeneo ya utaalamu na fedha ili kutekeleza mpango wa bima ya afya nchini.
“Kwa kuwa Serikali imeweka mazingira wezeshi ya wadau kushiriki katika maendeleo ya nchi, tutashirikiana na Serikali ikiwa ni pamoja na kutoa uzoefu tulioupata kutoka katika mataifa mengine ambayo yanatekeleza mpango wa bima ya afya kwa wote,” amesema Dkt. Abdulla.
Aidha, wadau wamepitishwa katika hatua ambazo Wizara imefikia katika utekelezaji wa mpango wa bima ya afya kwa wote ikiwemo tangazo la Serikali la kuanza kutumika kwa Sheria, kutungwa kwa Kanuni za Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote pamoja na utayari wa taasisi zitakazohusika katika utekelezaji ikijumuisha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)

Pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA)na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambao utahusika na utambuzi wa watu wasio na uwezo watakao gharamiwa na Serikali, kwani kiasi cha Shilingi Bilioni 173 kimetengwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kwa kuanzia kwa ajili ya kuwagharamia wananchi wasio na uwezo.
Mhariri:Harieth Kamugisha
0 Comments