Timu ya Tanzania Taifa Stars Imekubali kichapo cha Goli 1-0 kutoka kwa Timu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR. Congo) katika mchezo wa kufuzu fainali za kombe la Mataifa ya Afrika AFCON (2025) nchini Morocco.
Mchezo huo uliochezwa majira ya Saa 1:00 jion masaa ya Afrika masharika katika Dimba la Stade des Martyrs, Kinshasa nchini Kongo huku Timu ya kongo ikiibuka na ushindi huo wa goli moja alilojifunga Clement Mzize mnamo Dakika 53 wakati akiokoa mpira uliopigwa na mpinzani na kumshinda mlinda mlango Ally Salim Katoro nakupelekea mchezo huo kutamatika kwa dak 90 kwa 1-0.
Baada ya mchezo kutamatika kocha wa Stars Hemed Morocco amezungumza na baadhi ya wandishi wa habari waliosafiri na timu na kubainisha kuwa timu imecheza vizuri licha ya kupoteza hivyoa wanajipanga na mchezo wa marejeano huku akiahidi kufanyia marekebisho makosa yaliyojitokeza ili kuweza kupata matokeo mchezo wa nyumbani.
"Tunapaswa kusahau mechi iliyopita tuangalie mechi ijayo Tuna silu tatu za kujiandaa kwa ajili ya mchezo mwingine ninaamini Tutashinda mchezo wa nyumbani, mechi ilikuwa 50/50 hivyo yeyote angeweza kushinda tutafanyia kazi makosa yaliyojitokeza ili tuweze kupata ushindi mchezo ujao" Amesema Morocco kocha wa Stars.
Matokeo ya mchezo huo yanaifanya timu ya taifa la DR Congo kuongoza kundi H kwa Alama 9 ikifatiwa na Timu ya Tanzania yenye alama 4 huku Ethiopia wakishika nafasi ya tatu kwa alama 1 huku Guinea akiburuza mkia akiwa hana alama yoyote katika kundi hilo.
Mchezo wa marejeano utachezwa katika Dimba la Benjamin Mkapa siku tarehe 15 , 2024 huku Tanzania ikiwa na rekodi mbaya ya kutovuna alama zote dhidi ya Congo DR katika uwanja wa nyumbani takwimu za michezo mitatu ya mwisho katika dimba la Benjamin mkapa Dar Es salaam Stars amevuna alama 2 kati ya 9.
Ikiwa Taifa stars itafuzu itakuwa ni mara ya nne kushiriki katika fainali za michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika AFCON .
Mwandishi ; Sharifat Shinji
Mhariri:Harieth Kamugisha
0 Comments