Taifa stars yachapwa na Sudan huku ,Twiga stars waambulia sale dhidi ya Senegal



 Timu ya  Tanzania Taifa Stars imekubali kichapo cha goli 1-0 dhidi Sudani katika mchezo wa hatua ya kwanza wa kufuzu mashindano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani  CHAN 2024

ambapo itaanza kutimua vumbi mwezi Januari 2025 katika nchi tatu ambapo ni Tanzania, Kenya pamoja na Uganda  Taifa stars imepoteza katika uwanja wa ugenini Octoba 27, 2024 kwa bao 1-0 lililowekwa kimyani na

mchezaji Mohamed Abdel Raman anayekichapa katika timu ya Al-Hilal Omdurman mnamo dakika 23,mchezo wa marejeano utachezwa siku ya tarehe 3 Novemba katika Dimba la Benjamin Mkapa jijini Dares salaam.

Aidha kwa upande wa timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars wao wamelazimishwa sale ya 1-1 dhidi ya timu ya taifa ya wanawake ya Senegal katika mchezo wa kirafiki uliopangwa na shirikisho la mpira Duniani FIFA kwa ajiri ya maandalizi ya michuano ya mataifa ya Afrika kwa wanawake WAFCON msimu ujao.

Mchezo uliochezwa Octoba 27, 2024 huko nchini Morocco Twiga stars ilitangulia kupata goli mnamodakika ya 45+9 kupitia kwa Opa Clement kabla ya Senegal kupata Penalt manao dakika ya 90+9 nakuwekwa kimyani na Ndiaye Nguenar.



Ifahamike  kuwa timu za Taifa za Tanzania zimekuwa na mwendelezo mbaya wa matokea huku kwa timu ya taifaya wanaume Taifa Stars imekuwa na mfululizo mechi tatu bila kupata ushindi ikiwa imepoteza michezomiwili dhidi ya Kongo DR pamoja na mchezo dhidi ya sudan

Mwandishi:  sharifat shinji

Mhariri:  Abel mahenge


Post a Comment

0 Comments