Liverpool wapo katika mazungumzo ya kumuongezea mkataba Beki wa kimataifa wa Uingereza Trent Alexander-Arnold, 26. huku wakiwa kwenye mawindo ya kusaka sainiya Mholanzi wa Bayer Leverkusen Jeremie Frimpong, 23, Vanderson wa Monaco, 23, na Mtaliano wa Fiorentina, Michael Kayode, 20 kama mbadala endapo watashindwa kufikia malengo na kumpoteza beki huyo.
Liverpool wanapania kusaini mkataba mpya na mlinzi wa kati wa Uholanzi Virgil van Dijk mwenye umri wa miaka 33.
Kiungo wa kati wa Italia Jorginho, 32, anaangazia mustakabali wake Arsenal licha ya kuhusishwa na uhamisho wa Saudi Arabia.
Meneja wa zamani wa Chelsea Thomas Tuchel alitajwa kuwa ndiye anayetarajiwa kuwa mrithi wa Erik ten Hag wakati uongozi wa soka wa Manchester United ulipokutana mapema wiki hii.
Manchester City huenda wakamnunua mshambuliaji wa Sporting Lisbon na Uswidi Viktor Gyokeres, umri wa miaka 26,kama m-badala wa Haland ikiwa Barcelona watafanikiwa kumpata mshambuliaji wakimataifa wa Norway Erling Haland mwenye miaka 24, kutoka Etihad Man City.
Newcastle wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth na Ghana Antoine Semenyo, 24, huku kukiwa na ushindani kutoka kwa wapinzani wa Ligi ya Premia.
Kocha wa zamani wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amekataa ombi la kujiunga na timu ya taifa ya Denmark kwa sababu yuko kwenye mazungumzo na klabu kubwa kuhusu nafasi ya kocha mkuu.
Wolves wanafikiria kumnunua kocha wa Aberdeen Jimmy Thelin, iwapo wataamua kumfukuza Gary O'Neil.
West Ham wameanza mazungumzo juu ya mkataba mpya na mlinda mlango wa Uingereza Fin Herrick, 18.
Torino huenda wakamnunua mshambulizi wa kimataifa wa Argentina na timu ya Napoli Giovanni Simeone, 29, kufuatia mchezaji wa Colombia Duvan Zapata mwenye umri wa
miaka 33 kuandamwa na jeraha la goti.
Mwandishi: Eunice Jacob
Mhariri: Harieth Kamugisha
0 Comments