Tetezi za soko Ulaya Octoba 04, 2024

Paris St-Germain wameendelea kuweka juhudi za  kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Misri na Liverpool Mohamed Salah mwenye umri wa miaka 32, ambaye mkataba wake unamalizika  katika timu yake mwishoni mwa msimu huu.


Huku majogoo hao wa jiji la London Liverpool wakiwa tayari kutoa dau la paundi milioni 41 kumnunua fowadi wa Borussia Dortmund raia wa Ujerumani Karim Adeyemi mwenye umri wa miaka 22 kama mrithi wa Salah. 

Manchester United inaandaa ofa ya takriban paundi milioni 34 kumnunua winga wa Benfica na Uturuki mwenye umri wa miaka 25 Kerem Akturkoglu.

Newcastle United wapo kwenye harakati za kutaka kumnunua beki wa kati wa England Marc Guehi ,miaka 24 mwezi Januari 2025, huku wakitarajia  Crystal Palace  kumuuza mchezaji huyo.

Chelsea inahitaji kunasa Saini ya fowadi wa Colombia Jhon Duran, huku Aston Villa wakitangaza kuhitaji zaidi ya £80m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. 

Barcelona na Juventus wanafuatilia hali ya winga wa Argentina Alejandro Garnacho, miaka 20, huku mashetani wekundu Manchester United pia  wakimsajili  mchezaji huyo kwa paundi milioni 50.
                           Winga wa Argentina na Manchester united Alejandro Garnacho.

Atletico Madrid wanavutiwa na mlinzi wa Chelsea na England Ben Chilwell, 27, katika dirisha la uhamisho.

Newcastle United wako  mstari wa mbele kumsajili mshambuliaji wa Canada Jonathan David mwenye umri wa miaka 24 kutoka Lille.

Mshambuliaji wa Norway Erling Haaland, 24, anatazamiwa kusaini mkataba mpya na Manchester City lakini anataka kipengele cha paundi milioni 100 kiongezwe kwenye mkataba huo. 

Mwandishi:Eunice Jacob
Mhariri:Harieth Kamugishi 

Post a Comment

0 Comments