Upinzani nchini Georgia waitisha maandamano


  Picha: Irakli Gedenidze/REUTERS

Upinzani nchini Georgia umeitisha maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi huku Umoja wa Ulaya ukitaka uchunguzi ufanyike juu ya dosari zilizojitokeza, kufuatia matokeo ya uchaguzi wa bunge yaliyoibuwa mvutano.

Chama tawala kinachotuhumiwa kuegemea upande wa Urusi kimeshinda uchaguzi huo, ingawa Rais Salome Zurabishvili jana Jumapili aliituhumu Moscow kwa kuchochea udanganyifu kwenye uchaguzi huo.

Amesema kilichotokea ni operesheni maalum iliyoendeshwa na Urusi  Kutokana na madai ya upinzani wenye hasira, Rais Zurabishvili na rais wa zamani aliyeko jela Mikheil Saakashvili wameitisha maandamano ya umma.

Umoja wa Ulaya ulionya kwamba uchaguzi uliofanyika unatazamwa kama mtihani wa kidemokrasia katika taifa hilo ambao huenda ukaamuwa uwezekano wa Tbilisi kujiunga na jumuiya hiyo.

NA mwandishi wetu  


Post a Comment

0 Comments