Akizindua zoezi hilo katika mtaa wa Boma Mkuu wa Wilaya amesema kila mwananchi anawajibu wa kujiandikisha kwa mujibu na taratibu za nchi ili apate sifa ya kuchaguliwa au kumchagua kiongozi anayemtaka.
Amesisitiza kuwa kujiandikisha kunampa mwananchi fursa na haki ya kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 mwaka huu .
"Naomba kila mwananchi afahamu kuwa kujiandikisha katika daftari hili ni muhimu sana kwasababu unapata nafasi ya kuchagua kiongozi sahihi na zoezi hili liko kikatiba"
Aidha Kanali Mwakisu amesema TAMISEMI wametenga vituo 225 vya kujiandisha katika mji wa Kasulu Hivyo wananchi wafike kutimiza haki yao ya kikatiba.
Kwa upande wake msimamizi mkuu wa uchaguzi Halmasharu ya mji wa Kasulu Mwl.Vumilia Simbeye amewashukuru wananchi kwa kujitokeza katika uzinduzi huo,huku akiwataka wajitokeze kujiandisha katika zoezi linaloanza leo mpaka tarehe 20.
"Awali ya yote niwapongeze wananchi wa Kasulu kujitokeza kushiriki uzinduzi wa kujiandikisha kwenye daftari la kura la Serikali za mitaa, katiba yetu iko wazi na inamtaka kila mwanachi kushiriki kikamilifu"
Zoezi la Uzinduzi wa kujiandikisha kwenye daftri la mpiga kura serikali za mitaa Kitaifa limezinduliwa jijini Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe:Samia Suluhu Hassan.
Mwandishi : Abel Mahenge
Mhariri: Harieth Kamugisha
0 Comments