Ameyasema hayo leo Oktoba 29, 2024 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe. Maimuna Mtanda Mbunge wa Newala Vijijini aliyetaka kufahamu nilini Serikali itaanza ujenzi wa nguzo za Kilomita 2 katika Vijiji ambavyo mradi wa REA mzunguko wa Pili unatekelezwa.
Mhe. Kapinga amesema Kwa nyongeza ya umbali wa kilomita 2, REA kupitia Mkandarasi Central Electrical International Limite anaendelea na kazi na amefanikiwa kufikisha umeme kwenye vijiji 32 kati ya vijiji 76. Vijiji vilivyosalia vinatarajiwa kukamilika hivi karibuni.
Akijibu swali la Mbunge wa Kilombero, Mhe. Abubakar Asenga aliyeuliza lini Serikali itaunganisha umeme katika Kitongoji cha Upendo, Tupendane, Ikwambi na Misheni katika mji wa Ifakara, Mhe.Kapinga amesema vijiji hivyo vipo katika mradi wa vitongoji unaoendelea.
Akijibu swali la Mbunge wa Mbarali, Mhe. Keneth Ndingo aliyetaka kujua lini Vitongoji vya Igula A, Igula B na Mngolongolo vitapata umeme, Mhe. Kapinga amesema vijiji hivyo vimeshafanyiwa mapitio na vipo
katika mradi wa kupeleka umeme kwenye vitongoji 15 huku Mhe. Kapinga akisisitiza kuwa uunganishaji wa umeme utafanyika katika maeneo yote ya Vijiji.
Ifahamike kuwa dhamira ya Serikali kupitia kwa naibu Waziri wa nishat ni kuhakikisha wanachi wote wanapata nishati ya umeme na hivi sasa upo mradi wa Vitongoji 15 kwa kila jimbo na kuongeza kuwa upo mradi mwingine wa Vitongoji unaotarajiwa kuanza.
0 Comments