Polisi na Jeshi la Uganda UPDF limesema
jumatano kuwa Takribani watu 10 wamethibitishwa kufariki,na wengine 8 wamelazwa
hospitali baada ya kujeruhiwa katika shambulizi lililotekelezwa katika Wilaya
ya Kigadi,Magharibi mwa Uganda.
Polisi walisema washukiwa wawili pia
waliuawa walipokuwa wakijaribu kushambulia vikosi vya usalama.
Kwa mujibu wa Meja Bilal Katamba, Jeshi la Uganda na Polisi wameanza msako kuwabaini washukiwa wa shambulizi hilo wakati uchunguzi unaendelea.
Katika taarifa nyingine,msemaji wa polisi katika mkoa wa Albertine SP Julius Allan Hakiza aliwataja waliouawa miongoni mwao Watoto wanne,wengine 8 wamelazwa katika vituo vya afya huko Kyaterekera.
Jopo la maafisa polisi likiongozwa na DPC
Kagadi Ampurira Kenneth na maafisa wa Jeshi,wanashughulikia tukio hilo.
SP Hakiza amewasihi wananchi kutoa taarifa
zozote zinazohusiana na tukio hili kwakua Ushirikiano kati yao na vikosi vya
usalama ni muhimu ili kuwafikisha wahusika mbele ya sheria.
0 Comments