Takribani watu 78 wanahisiwa wamefariki dunia
na wengine kunusurika kifo baada ya feri kupinduka na kuzama katika Ziwa Kivu, mashariki mwa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Taarifa zinasema kuwa meli hiyo
iliyokuwa imewabeba abiria zaidi ya 278 na mizigo, ilizama muda
mfupi kabla ya kuwasili katika bandari ya mjini Goma ikiwa inatoka kwenye mji
wa Minova katika jimbo jirani la kivu kusini .
Kulingana na vyanzo vya ndani ,
meli hiyo kwa jina la Merdy, ilipinduka
saa nne asubuhi Octoba 3,2024 kwenye ziwa Kivu katika eneo la
umbali wa karibu meta 200 hadi kwenye soko kuu la kituku .
Watu wachache walionusurika
wamefikishwa mjini Goma wakiwa katika hali mahututi na wengine walifariki muda
mchache baada ya kufikishwa Hosptali
wakiwemo watoto wawili.
Nae gavana wa jimbo la Kivu kusini
Jean Jacques Purusi amesema Kulikuwa na abiria 278 ndani ya boti hiyo ,
Kwa mujibu wa BBC gavana wa mkoa huo amesema itachukua angalau siku tatu kupata idadi
kamili, kwa sababu bado miili yote
haijapatikana.
Mbali na abiria waliokuwemo, meli
hiyo pia ilikuwa imebeba shehena ya chakula na vifaa vingine muhimu kutoka
katika mji mdogo wa Minova jimboni kivu kusini.
Ziwa
kivu, ndilo limesalia kuwa njia pekee inayotumiwa kusafirisha bidhaa kwenda
katika mji wa Goma, tangu kufungwa kwa barabara na wapiganaji wa kundi la M23
miezi michache iliyopita
Ajali
hiyo imetokea ikiwa ni Miaka miwili iliyopita tangu ,
watu wasiopungua 55 kufariki dunia baada ya boti iliyojaza abiria kuliko uwezo wake
ilipozama kwenye mto kongo katika jimbo la mongala kaskazini mwa DRC .
Mwandishi: Ellukaga Kyusa
Mhariri: Harieth Kamugisha.
0 Comments