Magaba Sec yatamba kwa ubora mkoani Kigoma

Shule ya Sekondari Magaba mkoani Kigoma imetoa tuzo kwa wanafunzi wanaofanya vizuri zaidi katika masomo yao kama hamasa kwa watoto kielimu.

Tuzo hizo zimekabidhiwa wakati wa mahafali ya 11 ya shule hiyo yaliyofanyika Oktoba 2 mwaka huuq kwa wanafunzi sita waliofaulu mitihani katika masomo ya sayansi na kuipa heshima shule hiyo inayoongoza kwa ubora kitaaluma kwa shule binafsi.

Akikabidhi zawadi za vitabu vya sayansi vyenye thamani ya zaidi ya sh laki nne (400,000) Meneja wa Benki ya NMB Kasulu Bw. Ipyana Mwakatobe, amewapongeza wanafunzi hao kwa matokeo mazuri na kuhimiza jamii ya shule, wazazi na watoto wengine kuiga kutoka kwao.

Mwakatobe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo amewataka wazazi kuwalinda watoto dhidi ya matendo ya ukatili wa kijinsia yanayoendelea katika jamii nyingi.

"Wazazi jitahidini kudhibiti matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii kwa hawa wanaoingia uraiani, kwenye jamii kumekuwa na matendo ya ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kike na wakiume hivyo kaeni nao vizuri kwa kuwalinda juu ya matendo hayo" Amesema Ipyana.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Magaba Ndg. Emmanuel N'ghulu akitoa taatifa ya maendeleo ya shule amejivunia mafanikio makubwa ya kitaaluma akiitaja Magaba kama kituo sahihi cha elimu na malezi

Mwalimu N'gulu ameeleza kuwa shule hiyo inafanya vizuri katika mitihani ya wilaya na mkoa kwa kushika nafasi ya kwanza kiwilaya na nafasi ya 14 kimkoa kati ya shule 197 kwa mwaka 2024.

Amesisitiza kuwa matarajio yao kwa wanafunzi wanaohitimu kufaulu kwani walimu wamejitoa kwa kufundisha kwa nadharia na vitendo ili kuwajenga katika kujibu mtihani wa wa mwisho wa kuhitimu kidato cha nne mwaka 2024.

"Tunamatarajio makubwa kwa wahitimu wa mwaka huu kuongeza kiwango cha ufaulu zaidi na kupata nafasi ya juu kimkoa na kitaifa kwani walimu wamejituma kuwandaa wanafunzi wao kuelekeam chumba cha mtihani" Amesema N'ghulu.

Aidha amewahimiza wazazi na walezi kulipa ada na michango kwa wakati ili kuiwezesha shule kutoa huduma stahiki kwa wanafunzi ikiwemo ufundishaji na malezi.

Awali, akisoma Risala kwa niaba ya wanafunzi wa kidato cha nne 2024 Modesta Fanuel ameishukuru shule kwa ubora wa ufundishaji unaowawezesha kupata taaluma na ujuzi.

Hata hivyo amekiri kuwepo kwa changamoto ya mwamko hafifu wa wazazi katika suala la elimu.

"Wazazi na walezi wamekuwa na mwamko hafifu katika suala la elimu, wengi hawapo tayari kuwanunulia watoto wao vifaa mhimu vya vya kujifunzia kama vile vitabu vya kujifunzia" Amesema Modesta Fanuel.

Nae Mkurugenzi na mmiliki wa shule hiyo Ndg. Leonard Reuben Magaba amewaomba wazazi kuwapokea watoto watakapomaliza mitihani yao na kuwahimiza kufanya kazi za mikono, kuwaonya na kuwaelekeza juu ya athari za matendo maovu kwenye jamii.

"Hawa watoto watakapomaliza mitihani yao wakija nyumbani mkae nao vizuri, muwahimize kufanya kazi kazi, muwafundushe kuwa na tabia njema, muwaonye na kuwaelekeza wala wala wasiwashinde" Amesema Magaba.

Pichani  katikati ni mgeni rasimi wa mahafali ya 11 Ndg. Ipyana Mwakatobe, kulia ni Mkurugenzi wa shule ya sekondari Magaba Ndg.Leonard Reuben Magaba  na kushoto ni Mkuu wa shule hiyo Ndg. Emmanuel N'ghulu.

Shule ya Magaba imeanzishwa mwaka 2011chini ya mjasiriamali Leonard Reuben Magaba na kusajiliwa rasmi na mamlaka za elimu tarehe 16/11/2011 kwa usajili wa namba S.4524 na kupewa ithibati ya kuwa kituo cha mtihani kwa namba S.4810 kwa wanafunzi waliopo shuleni na P.4810 kwa wanafunzi wa kujitegemea 

Mwandishi; Eunice Jacob  

Mhariri; Sharifat Shinji

Post a Comment

0 Comments