Wilaya ya Kasulu yafanikiwa kuvuka lengo la uandikishaji

Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma imefanikiwa kuvuka lengo la uandikishaji wa  orodha ya Daftari la  mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa katika halmashauri zote za wilaya hiyo.

 

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Octoba 21 2024, msimamizi wa uchaguzi  halmashauri ya wilaya ya Kasulu Dkt. Semistatus Mashimba amesema licha ya kukabiliwa  na Changamoto za umbali wa vituo vya uandikishaji walifanikiwa kuongeza vituo vya uandikishaji kwa ajili ya kuwafikia walengwa wote waliokusudiwa na kufanikiwa kufikia malengo waliyojiwekea.

 

Dkt.Mashimba amewapongeza wananchi, viongozi wa siasa, viongozi wa dini pamoja na vyombo vya habari kwa kutoa elimu kwa wananchi na kufanikisha zoezi hilo huku  kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura ambayo itakuwa tarehe 27 Novemba 2024,katika kituo ulichojiandikishia.


Hata hivyo Dkt Mashimba hakuwa tayari kutaja takwimu za matokeo ya uandikishaji katika hamashauri yake akidaikuwa hana mamlaka hayo.

 

Orodha ya wapigakura itabandikwa leo tarehe 21/10/2024 kwenye mbao za matangazo na msimamizi wa uchaguzi ili kuwezezesha wananchi kukagua wapiga kura kwa ajili ya usahihi wa orodha hiyo, Kurekebisha jina la mpiga kura, kubadilisha taarifa iliyopo kwenye orodha hiyo na kufuta jina lililo orodheshwa kwa vile aliyeorodheshwa  amekosa sifa za mpiga kura, zoezi la ukaguzi wa orodha ya wapiga kura litaendelea mpaka tarehe 27/10/2024 siku ya Jumatano.


Mwandishi: Ellukaga Kyusa


Mhariri :Harieth Kamugisha

Post a Comment

0 Comments