Kanisa la Kiangalikana nchini Kenya wameishutumu serikali ya Raisi Willium Ruto kwa kutotekeleza ahadi zake kwa wananchi.
Hayo yameelezwa na kundi la viongozi wa kidini wa Kanisa la Kiangalikana eneo la Nyanza Magharibi ya Kenya na kutangaza kufanya maombi ya kitaifa kulaani kile kinachoendelea nchini na pia dhidi ya viongozi wa kisiasa wanaoshiriki ufisadi.
Viongozi hao wa kidini ambao wamesisitiza kuwa, kamwe hawatotishwa na vitisho wameendelea kuishinikiza serikali kuongeza juhudi zinazotumika katika masuala binafsi ya viongozi wa kisiasa mfano nguvu iliyowekwa kumuondoa aliyekuwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua kutatua changamoto zinazowakabili Wakenya.
Kufuatia msimamo huo wa Kanisa la Kiangalikana, kundi moja la viongozi wa kanisa hilo pia kutoka eneo la Nyanza Magharibi mwa Kenya wakiongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Maseno Magharibi, John Mark Godia wamesimama na kauli ya wenzao wa Kanisa Katoliki ambao pia waliikosoa serikali hiyo na kusema Mheshimiwa Sholei anastahili kupunguza kujipiga kifua na matamshi dhidi ya watu anaowataja kuwa wanaoipinga serikali.
" wanastahili kupunguza kasi yao kuwakabili maaskofu wa Kikatoliki na viongozi wa kanisa pindi wanapozungumza dhidi ya ufisadi nchini" alisema Askofu Godia sauti ya kuwatetea wanyonge.
Habari;Ellukagha kyusa.
Mhahir:Eunice Jacob.
0 Comments