Waandishi wa
habari toka Mikoa sita yaKanda ya Ziwa wamejengewa uwezo na Banki Kuu Tawi la
Mwanza ili waweze kuandika habari za uchumi na fedha kikamilifu.
Mkurugenzi
wa Tawi la Banki Kuu Kanda ya Ziwa Bi Gloria Mwaikambo wakati wa kufungua
mafunzo hayo ya siku mbili alisema kuwa, mafunzo hayo yanalenga kujenga uelewa
Kwa kundi la waandishi wa habari ili waweze kuandika habari za uchumi na fedha
Kwa weledi zaidi.
Pia Bi
Mwaikambo aliongeza kuwa mafunzo hayo pia yatawaleta waandishi karibu na Benki
kuu ili waweze kuelewa zaidi shughuli za Benki kuu.
Katika mafunzo haya ya siku mbili mtapitishwa
kwenye kujua muundo na majukumu ya Benki kuu, umuhimu wa Benki Kuu kuwa na
dhahabu kama sehemu ya akiba, utekelezaji na sheria na kanuni za huduma ndogo
za fedha na mada nyingine mbalimbali" alisema Bi Mwaikambo.
Pia
aliongeza kuwa mafunzo hayo yameshafanywa kwenye matawi mbalimbali ya Benki kuu
na sasa ni zamu ya Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Nanye
Mwenyekiti wa mafunzo hayo Bwana Edwin Soko aliishikuru Benki kuu kuleta
mafunzo hayo Kwa kuwa yatakwenda kuwafanya waandishi hao kuandika habari za
uchumi na fedha Kwa weledi.
Pia Soko
aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa mabalozi wazuri wa kuandika habari za
Benki kuu Kwa weledi.
Mafunzo hayo
yamejumuisha idadi ya waandishi wa habari arobaini toka Mikoa ya Mwanza,
Simiyu, Geita, Kagera, Simiyu na Shinyanga.Mafunzo hayo yamefanyika kwenye
ukumbi wa mkutano wa Benki kuu Tawi la Mwanza, Jijini Mwanza.
Mwandishi:Ellukagha Kyusa.
Muhariri: Prosper Kwigize.
0 Comments