COP29 yakosolewa na wanaharakati wa zamani wa masuala ya hali ya hewa.

Wanaharakati wakipinga ushawishi wa mawakala wa uchimbaji mafuta na gesi wakati wa mkutano wa COP29 huko Baku,Azerbaijan.

Kundi la Viongozi wa zamani na wataalamu wa Masuala ya hali ya hewa wamekosoa mazungumzo yanayoendelea katika mkutano wa Umoja wa wataifa Cop29 kuwa hayakidhi malengo yaliyoweka hapo awali.

Viongozi hao wamesema kupitia barua ya wazi iliyotiwa saini na viongozi mbalimbali wa zamani na kubainisha kuwa utaratibu wa COP  29 umefikia pakubwa lakini sasa unahitaji mabadilko makubwa.

Barua hiyo iliyotiwa saini na wataalamu 20, viongozi wa zamani na wanasayansi akiwemo mkuu wa zamani wa UNFCCC, Christine Figueres na katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon, na rais wa zamani wa Irelanda Mary Robinson wanasema yanahitaji kufanyiwa mageuzi.

Hata hivyo mkutano huo umekuwa na mgawanyiko baada ya mawakala wa uchimbaji wa mafuta na Gess kuwa na mitazamo yao tofauti ya kuendelea kutetea upande wao ingawa tafti zinaonyesha uchimbaji wa mafuta na gesi vimekuwa ni vyanzo vya kusababisha mabadiliko ya Tabianchi

Kupitia taarifa iliyoripotiwa na VOA takriban nchi 200 zinakutana Baku, Azerbaijan kwa azma kuu ya kukubaliana juu ya lengo jipya ni kiasi gani cha pesa kinahitajika kuzisaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Ifahamike kuwa mkutano wa Cop 29 unalenga kuzisaidia nchi mbalimbali zinazokabiliwa na mabadiliko ya hali ya hewa ili kuweza kumudu mabadiliko hayo.

Mhariri; Sharifat Shinji


Post a Comment

0 Comments