Dkt. Biteko apongeza Kanisa Katoliki kwa kuunga mkono serikali

 


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Serikali imeendelea kutekeleza miradi mingi katika sekta ya afya inayolenga  kuongeza ufanisi katika huduma za afya na kuboresha maisha ya Watanzania.

Dkt. Biteko amesema hayo leo wilayani Sengerema wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa jengo la jipya la kisasa la upasuaji  na mradi wa umeme wa jua katika hospitali ya Sengerema DDH iliyopo chini ya Kanisa Katoliki, Jimbo Katoliki la Geita.

Akitaja baadhi ya mafanikio ya Serikali katika sekta hiyo Dkt. Biteko amesema  Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Samia  imefanya kazi nyingi ikiwemo kujenga hospitali mpya 129, kukarabati hospitali kongwe 50, kujenga hospitali za wilaya 677 na zahanati 425. 

Dkt. Biteko amewashukuru wafadhili wa miradi hiyo na kuifanya hospitali hiyo kuwa bora na ya kisasa na kulipongeza Kanisa Katoliki kwa kufanya umisionari unaolenga kuhudumia watu kiroho na kimwili.

Mhasham Askofu Flavian Kassala wa Jimbo Katoliki la Geita


Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Katoliki Geita, Flavian Kassala amesema hospitali ilijengwa kufuatia ujio wa watawa sita na familia moja waliohitaji kujenga hospitali ambayo ingetoa huduma ya afya kwa wahitaji na baadaye hospitali hiyo ikawa teule hadi mwaka huu ambapo Serikali imejenga hospitali yake ya wilaya.


Post a Comment

0 Comments