Mjumbe Wa mkutano mkuu Taifa wa chama cha Mapinfuzi CCM Mhe Christopher Gachuma amemuwakilisha Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Miungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ambaye ni Mlezi wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Kigoma katika Uzinduzi wa Kampeni za CCM wilaya ya Kasulu.
Mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni umefanyika katika uwanja wa Mpira Kiganamo katika Halmashauri ya Mji Kasulu huku akiwataka wagombea kufanya kampeni za kweli ili waendelee kuitetea bendera ya Chama Cha mapinduzi katika mkoa huo.
"Nimewasikia wabunge wote na kila mmoja ametaja miradi iliyotekelezwa katika majimbo yenu na kila mmoja amejinadi hapa na wananchi mmesikia kwa hiyo sina mengi ya kuwambia wala mapya maana wabunge wameyasema hapa wote tumesikia" Amesema Gachuma.
Aidha amewaomba wananchi kujitokeza siku ya Uchaguzi ili kupiga kura na kuwatoa wasiwasi wananchi kuhusu CCM kuwa itaendelea kuboresha miundombinu, kutekeleza kile ambacho wanakiahidiwakati wa kunadi sera zao.
"Ndugu zangu wananchi siku ya Tarehe 27, Novemba jitokezeni mpige Kura itakuwa ni ajabu kama hamtajitokeza siku ya uchaguzi nendeni mkapige kura na muwapigie kura viongozi wenu wa mitaa tunatambua serikali za mitaa ndo chanzo cha maendeleo"
Katika hatua nyingine Mbunge wa Jimbo la Kasulu mjini Prof. Joyce Ndalichako amesema Chama cha mapinduzi kimejipanga kuchukuwa ushindi kila kata huku akitaja Miradi iliyotekelezwa na Ilan ya chama cha mapinduzi CCM katika Halmashauri ya Mji kasulu.
"Sisi tushamaliza uchaguzi kwa sababu tulianza maandalizi mwaka 2020 baada ya kupewa kijiti tulianza kutekeleza miradi tumejenga shule za Sekondari 8, Tumejenga shule za msingi 5 pamoja na kutekeleza miradi mingine mfano mradi wa maji, pamoja na wizara ya afya" Amesema Ndalichako.
Ndalichako ameongeza kuwa serikali imeshatoa pesa kwa ajili ya ujezi wa shule ya sekondari katika kata ya Mrusi mkombozi pamoja na ujenzi wa shule ya msingi kata ya Kanaza katika halmashauri ya Kasulu mji .
"Serikali kupitia kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dakt. Samia Suluhu Hassani, nimepokea pesa Milioni 603 kwa ajili ya sekondari kata ya Mrusi Mkombozi pia nimepokea pesa milioni 354 Kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi kata ya Kanaza" Amesema Ndalichako.
Kwa upande wao Wananchi wilayani humo wamewaomba wagombea kutimiza ahadi zao watakazo ahidi wakati wa kampeni kama wakichaguliwa kuongoza katika maeneo yao ambayo wamechukua fomu kwa ajili kuwania nafasi mbalimbali katika uongozi wa serikali za mita.
Naye ndg Fider Elias Manyanya amesema kuwa kwa upande wa ahadi wanazo zinadi wagombea wakiwa kwenye majukwaa ni wajibu wao kuzitimiza kwa wanachi ili waweze kuwapatia wanachoitaji.
Mikutano ya kampeni ndio sehemu ya kila mgombea kunadi sera zake alizo nazo na mipango yake ya maendeleo kwa wananchi ili waweze kumchagua kiongozi bora mwenye kuleta maendeleo.
Mwandishi: Sharifat Shinji
Mhariri:Eunice Jacob.
0 Comments