Hezbollah warusha roketi 250 kuvuka Lebanon.

Jeshi la Israel imesema takribani roketi 250 zimerushwa na Hezbollah kuvuka mpaka kutoka Lebanon, na kuashiria moja ya mashambulizi makali zaidi ya Israel tangu mapigano yalipozidi mwezi Septemba.


Polisi wa Israel walisemaWatu kadhaa walijeruhiwa na majengo kuharibiwa kaskazini na kati mwa Israel, baadhi yao wakiwa karibu na Tel Aviv .

Mashambulizi hayo yalifuatia shambulizi la anga la Israel katikati mwa Beirut siku ya Jumamosi, ambapo wizara ya afya ya Lebanon ilisema watu 29 waliuawa.

Pia siku ya Jumapili vyombo vya habari vya Israel viliripoti kwa wingi kuwa Israel na Lebanon zinaelekea kwenye makubaliano ya kusitisha mapigano ili kumaliza mapigano na wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran, Hezbollah.

Kufuatia mashambulizi makali kutoka Lebanon, polisi wa Israel wamesema kuwa wamepokea taarifa za vifusi vya roketi kuanguka katika eneo la Tel Aviv.

Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilisema shambulio la moja kwa moja katika kitongoji kimoja limeacha "nyumba zikiteketea na magofu".

Roketi zilianguka katika Petah Tikva, karibu na Tel Aviv, na katika baadhi ya maeneo ya kaskazini: Haifa, Nahariya na Kfar Blum, vyombo vya habari vya Israeli viliripoti.

Hezbollah, ambayo hapo awali iliapa kujibu mashambulizi dhidi ya Beirut kwa kulenga Tel Aviv, ilisema kuwa ilirusha makombora ya katika maeneo mawili ya kijeshi katika mji huo na jirani.

Baadaye, IDF ilisema ilikuwa imekamilisha mashambulizi kwenye vituo 12 vya kamandi vya Hezbollah huko Dahieh, ngome ya kundi hilo katika vitongoji vya kusini mwa Beirut.

Wizara ya afya ya Lebanon siku ya Jumapili iliongeza idadi ya vifo kutoka 20 hadi 29 kutokana na shambulizi kubwa la Israeli liliioanzishwa bila ya onyo katikati mwa Beirut. Ilisema jumla ya watu 84 waliuawa nchini humo siku ya Jumamosi.

Mwandishi:Eunice Jacob.
Mhariri:Abel Mahenge.

Post a Comment

0 Comments