Idadi ya watu waliofariki kariakoo kwa kuporomoka ghorofa yafikia 29


 Idadi ya waliofariki  kutokana na kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika soko kubwa la kibiashara Kariakoo, Dar es Salaam, imefikia watu 29 baada ya miili tisa kupatikana.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba akizungumza na vyombo vya habari leo, amesema miili hiyo tisa imepatikana wakati wa shughuli za kuondoa kifusi.

Aidha  Makoba amesema  shughuli za uokozi zimefikia tamati leo Jumanne Novemba 26.

Jengo hilo liliporomoka asubuhi ya Jumanne Novemba 16, 2024 huku zaidi ya watu 80 wakiokolewa wakiwa hai.

Mwandishi : Harieth Dominick 

Post a Comment

0 Comments