Kukua kwa uchumi kwa mkoa wa dar es saalamu vyatajwa kuongeza mahitaji ya umeme



 Ukuaji wa kasi ya maendeleo na uchumi katika Mkoa wa Dar es Salaam unachangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa ongezeko la mahitaji ya umeme.

Amezungumza hayo leo Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga wakati wa ziara yake iliyolenga kukagua maendeleo ya maboresho ya miundombinu ya umeme katika kituo cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam iki kukiongezea uwezo.

Amewatoa hofu wakazi wa Dar es Salaam na Pwani hususani Gongo la Mboto, Dege na Mkuranga kuwa Tanesco imekamilisha maboresho iliyokuwa ikifanya siku tatu zilizopita na tayari transfoma zimefungwa na hivyo kupunguza mzigo kwenye vituo vya Mbagala Ubungo, Dege na Gongo la Mboto.

Amesema kwa sasa kasi ya ukuaji  wa Mkoa wa Dar es salaam ni takriban asilimia 16 huku mahitaji ya umeme yakiongezeka kutokana na shughuli za kiuchumi na ndio maana Tanesco imekuja na mpango wa maboresho ya miundombinu pamoja na njia za kusafirisha umeme ili kukidhi mahitaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mha. Gissima Nyamo-Hanga amesema hatua zinazochukuliwa ni pamoja na kuboresha njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 220 kutoka Kimara-Ubungo-Mabibo hadi Ilala na ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Mabibo ili kupunguza mzigo kwenye kituo cha Ilala.

Mkoa wa Dar es Salaam unapata umeme kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo Gesi Asilia ambapo mahitaji ya umeme ni wastani wa Megawati 602 huku Mkoa wa Pwani mahitaji yakiwa Megawati 136 na hivyo kufanya ukanda wote wa Pwani na Dar es Salaam kuwa na mahitaji ya megawati 738.

Mwandishi: Mussa Mkilanya 

Mhariri ;Abel Mahenge 









Post a Comment

0 Comments