Kitengo cha kufuatilia makubaliano ya kusitisha vita kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wanaoungwa mkono na Rwanda M23, kitazinduliwa rasmi Jumanne.
Siku ya Ijumaa, Angola ilisema kuwa itaongoza kitengo hicho cha kufuatilia mkataba wa kusitisha mapigano Kongo kitakachowajumuisha maafisa wa Kongo na Rwanda.
Waasi wa M23 wameteka maeneo kadhaa mashariki mwa Kongo
Waasi hao wa M23 wengi wao kutoka kabila la Watutsi, wameteka maeneo kadhaa ya mashariki mwa Kongo inayokabiliwa na ghasia tangu mwaka 2021 na kuwalazimu maelfu ya watu kukimbia makazi yao na pia kusababisha mzozo wa kibinadamu.
Angola yaituhumu M23 kwa kukiuka usitishaji mapigano Kongo.
Makubaliano ya kusitisha mapigano yaliotiwa saini mwezi Agosti yalileta utulivu katika uwanja wa vita, lakini tangu mwishoni mwa mwezi Oktoba, kundi hilo la M23, limekuwa likifanya mashambulizi katika jimbo la Kivu Kaskazini kuelekea katika mji wa kimkakati wa Pinga.
0 Comments