Makamu wa raisi Kamala akubali kushindwa uchaguzi urais.

 

Mpinzani mkuu wa Trump katika uchaguzi wa Novemba 5, Makamu wa Rais Kamala Harris alitoa hotuba ya kukubali kushindwa mbele ya maelfu ya wafuasi wake katika Chuo Kikuu cha Howard .

Kwanza, kama ilivyo kwa utamaduni uliozoeleka kwenye mataifa ya kidemokrasia, Bi,Harris alimpigia simu Trump kukubali kushindwa na kumpongeza rais huyo wa zamani wa Marekani kwa ushindi aloupata utakaomrejesha ikulu ya White House kwa miaka mingine minne.

Kwenye hotuba yake ya kukubali kushindwa, Harris amewarai Wamarekani "kutokata tamaa" akiwataka waendelee "kupambana".

"Ingawa ninakubali kushindwa kwenye uchaguzi huu, lakini sikubali kuitelekeza shauku ya kupambana iyoitia nguvu kampeni yangu alisema Harris katika sehemu ya hotuba yake aloitoa mbele ya majengo ya Chuo Kikuu cha Howard.

Mwanasiasa huyo ambaye iwapo angeshinda angekuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani, amesema yeye na rais Joe Biden watafanya kila wawezalo kuhakikisha ubadilishanaji madaraka kwenda kwa Trump unafanyika kwa njia ya amani.

Ahadi hiyo imeonesha utofauti mkubwa na kile kilichotokea miaka minne iliyopita, pale Trump alipokataa kukubali kushindwa uchaguzi na Joe Biden, na  kusababisha wafuasi wake kuvamia majengo ya bunge mjini Washington.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump ashinda uchaguzi kwa muhula mwingine wa miaka minne.

Donald J. Trump ndiye rais mpya wa marekani akishinda kura za kutosha za wajumbe maalum wa majimbo ,Alishinda majimbo muhimu kama Pennsylvania, Georgia, North Carolina, na Wisconsin. Awali, alikuwa rais kuanzia mwaka 2017 hadi 2021.

Wafuasi wanamchukulia rais huyo wa Republican kama mwokozi na shujaa, aliyekuwa tayari kutetea maadili yao dhidi ya waliberali nchini Marekani. 

Wakosoaji wanasema ni mhalifu aliyeshtakiwa, na walifuatilia kampeni kwa mshangao na kueleza kushtushwa na siasa zake kali, mienendo isiyo ya kiserikali, na matumizi yaliopindukia ya mitandao ya kijamii ndani na nje ya ofisi.

Katika kampeni za uchaguzi wa 2024, Trump alitoa kauli kwamba wahamiaji wa Haiti huko Springfield, Ohio, walikuwa wakiiba paka na mbwa wa majirani ili kuwala, madai ambayo yalithibitishwa kuwa ya uwongo.

Uchungzu mkubwa ulithibitisha kuwa madai hayo si ya kweli. Hata hivyo, Trump alishikilia hadithi kwamba Wademocrat walifanya udanganyifu katika uchaguzi licha ya mahakama zote ambazo madai kama hayo yalitolewa kutupilia mbali tuhuma hizo.

Mnamo Januari 6, 2021, kundi la wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia na wafuasi wa Trump walivamia Jengo la Capitol linalohifadhi bunge la Marekani mjini Washington, DC, katika jaribio la kuzuia uthibitisho rasmi wa ushindi wa Biden.

Ingawa inachokingoja Marekani na dunia nzima wakati wa muhula wa pili wa Trump hakitabiriki, kuangalia nyuma kwenye muhula wake wa kwanza kunaweza kutoa maarifa fulani kuhusu kitakachokuja.


Post a Comment

0 Comments