Ripoti hiyo imetolewa na UNESCO kupitia kwa mkurugenzi wa taasisi hiyo Audrey Azoulay leo jumamosi ya November 2, 2024 na kusema kuwa ongezeko hilo la mauaji ya waandishi wa haabari linatia hofu kwani hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa karibia visa vyote hivyo vya mauaji.
Azoulay ameyataka mataifa duniani kuongeza juhudi kuhakikisha kwamba wanaotenda vitendo hivyo vya kuwauwa waandishi wa habari wanachukuliwa hatua za kisheria. UNESCO imesema kuwa idadi kubwa ya waandishi waliuwawa katika maeneo yenye mizozo mwaka 2023, ni waandishi 44 walipoteza maisha, ikiwa mara ya kwanza tangu mwaka 2017 ambapo idadi ya waandishi wa habari waliofaliki katika maeneo kama hayo ilikuwa inapungua.
Kulingana na UNESCO maeneo ambayo hayana hatari kubwa kwa waandishi ni Amerika Kaskazini na Ulaya Magharibi ambapo waandishi 6 pekee ndio waliouwawa katika kipindi hicho cha miaka miwili.
Kamera ya mwandishi aliyejeruhiwa na bomu katika vita vya Mashariki ya Kati : picha Hassan Ammar photo/picture Alliance
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa UNESCO Audrey Azoulay amesema kuwa kati ya nchi 75 ambazo UNESCO iliwasiliana nazo kwa ajili ya kupata idadi za waandishi waliouwawa, 17 hazikutoa majibu kabisa na nchi 9 zilikubali ombi hilo ila hazikutoa jawabu.
Kila ifikapo Novemba 2 kila mwaka UNESCO hufanya kampeni ya kuuhamasisha umma dhidi ya unyama wa kuuwawa kwa waandishi wa habari ambapo mwaka huu shirika hilo la Umoja wa Mataifa litafanya mkutano kuhusiana na usalama wa waandishi wakati wa kuripoti kuhusiana na mizozo. Mkutano huo utafanyika katika Mji Mkuu wa Ethiopia Addis Ababa mnamo Novemba 6.
Mwandishi; Ramadhan Zaidy
Mhariri; Sharifat Shinji
0 Comments