Maandamano yamezuka nchini Israel baada
ya Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu kumfuta kazi Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo
Yoav Gallant.
Netanyahu amesema "mgogoro wa uaminifu" kati ya viongozi hao wawili ndio uliosababisha kuchukua uamuzi huo, akiongeza kuwa imani yake kwa Gallant "imepungua" katika miezi ya hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Nje, Israel Katz ataingia kuchukua nafasi yake.
Kufuatia habari hizo, Gallant alichapisha taarifa kwenye mitandao ya kijamii akisema "usalama wa taifa la Israel ulikuwa na utabaki daima kuwa ndio misheni ya maisha yangu."
Katika siku za nyuma alisema mpango wa kuwarudisha nyumbani waliotekwa nyara na Hamas, unapaswa kupewa kipaumbele hata kama itamaanisha kuingia makubaliano kuhusu vita vya Gaza.
Netanyahu na Gallant kwa muda mrefu
wamekuwa na uhusiano wa kikazi wenye mgawanyiko.
Katika kipindi cha mwaka uliopita, kumekuwa na
ripoti za kuzozana kati ya watu hao wawili kuhusu mkakati wa vita wa Israel.
0 Comments