Mhe: Joyce ndalichako awataka wagombea wa CCM Mjini Kasulu kuepuka Lugha za matusi katika kampeni

 

Mbunge wa jimbo la Kasulu mjini mkoani Kigoma Mhe: Joyce ndalichako ametembelea kata ya heru juu,msambara  kuzungumza na wagombea walio teuliwa kwa tiketi ya chama cha mapinduzi(CCM) na kuwataka kujiamini na kujiandaa vyema  kwa kampeni.

Ziara hiyo ameifanya Novemba 14,2024 baada ya kukutana na kamati ya utekelezaji ya Mkoa na Wilaya mjini Kasulu. 

 

Mhe: Ndalichako amewataka wagombea kuwepuka kutumia lugha za matusi,vurugu, na kuondoa makundi ndani yao ili kupata uongozi mahiri na imara wa kuunga mkono kazi zinazotekelezwa na serikali ya awamu ya sita.

"Nawakumbusha tunaelekea kwenye kampeni hivyo nawaomba tujiamini na tusitumie Lugha za matusi ili kupata viongozi wenye Busara na Hekima "


Kwa upande wa katibu wa UWT mkoa sarah kairanya amesema lengo la kamati ya utekelezaji uwt mkoa na wilaya ni kuhamasisha uchaguzi wa serikali za mitaa,ushirikiano kwa wagombea.


 Nao baadhi ya wagombea wateule wamewasilisha changamoto zinazoikabili mitaa na kata kuwa ni ukosefu wa umeme, changamoto ya maji safi mtaa wa mwanga,ukosefu wa wodi ya wazazi katika zahanati ya muungano na kuiomba serikali kutatua kero hizo zinazo wakabili.

"Tunachangamoto ya ukosefu wa wodi ya wazazi katika Zahanati ya Muungano Tunaomba serikali itusaidie tupate zahanati"


Wamemshukuru mbunge wa jimbo la Kasulu mjini kwa jitihda za kuleta maendelea ndani ya kata zao na kutatua changamoto ya miundombinu ya barabara.

 Kampeni za wagombea wa ngazi mbalimbali za uongozi wa serikali za mitaa utafanyika november 20 huku uchaguzi ukitarajiwa kuwa ni november 27 mwaka huu.

Mwandishi:Eunice Jacob

Mhariri:Harieth Dominick 


Post a Comment

0 Comments