Akizungumza wakati wa uokoazi, Mkuu wa jeshi la zimamoto Wilaya ya Kasulu,(SGT)Africanus Mrema amesema Tukio hilo limetokea saa 9 Usiku kuamkia Novemba 29 kwenye mtaa huo,Ambapo inatajwa chanzo cha tukio hilo ni mgogoro uliokuwa ukiendelea kati ya wanandoa hao.
"Kwa uchunguzi wa awali wamebaini chanzo cha tukio ni mgogoro uliokuwepo kati ya wanandoa hao kutokana na mwaname kuwa mlevi na kuacha majukumu yote ya ulezi na matunzo ya watoto kwa mwanamke huyo" amesema Sajenti Mrema
Theodora Musa ambaye ni manusura wa ajali hiyo amesema Chanzo na ugomvi ni kumshauri mumewe kutafuta kazi ili aweze kumsaidia jukumu la kutunza familia,Jukumu alilokuwa ametelekezewa na mumewe.
Theodora Musa Manusura wa Tukio hilo akiwa ndani ya nyumba iliyochomwa moto,mtaa wa Mkapa kata ya Kumnyika Halmashauri ya Kasulu mji.
"Nilimwambia atafute kazi ili tusaidiane kulea watoto kwasababu ameniachia mimi majukumu yote ya malezi yeye analewa ,Ndo akakasirika na kuamua kuchoma nyumba nikiwa ndani"Alisema Theodora.
Bi, Vumilia Sanda na Suleiman Rashid ni mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa walisikia sauti saa tisa usiku ikilia kuomba msaada ndipo walipo chukiwa hatua ya kutoa msaada wa uokozi kwa kujaribu kuzima moto huo kwa kutumia maji.
Hata hivyo mkuu wa Jeshi la Zimamoto amesema walikuta dumu la petro eneo la tukio.
Mwandishi:Eunice Jacob.
mhariri:Harieth Dominick
0 Comments