Mkuu wa Wilaya ya Kasulu,Mkoani Kigoma , Mhe Kanali Isack Mwakisu amepiga kura ya kuchagua kiongozi wa serikali za mitaa katika kituo cha Boma ,Kata ya Kimobwa na kuwa ahakikishia wananchi usalama katika vituo vyote vya kupiga kura .
"Kama Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya Hali ya usalama umeimarishwa vyema na tunategemea uchaguzi kuisha kwa amani ndani ya muda uliopangwa na wizara husika" Amesema kanal Mwakisu.
Aidha Kanali Mwakisu amepongeza mwitikio wa wananchi huku akiwasihi kuendelea kurejea katika maeneo yao,Kudumisha utulivu na Amani baada ya kupiga kura.
Msimamizi wa uchaguzi Halmashauri ya mji Kasulu Mwl.Vumilia Simbeye akipiga kura kituo cha Boma ,Kata ya Kimobwa,MjiKasulu.
Kwa upande wake msimamizi wa uchaguzi Halmashauri ya mji Ksaulu Mwl.Vumilia Simbeye ambae pia amepiga kura katika kituo hicho amsema ametembelea vituo vyote 118 na zoezi linaenda vizuri.
Aidha Mwl.Simbeye amesema utaratibu umewekwa vizuri na kila changamoto itakayojitokeza,itapatiwa uvumbuzi ili kuhakikisha kila mwananchi mwenye haki ya kupiga kura anafanya hivyo .
"Utaratibu uko vizuri kabisa,hata watu wenye ulemavu wanapata kipaumbele cha kupiga kura katika vituo vyao na wasioona majina yao watawasiliana na wasimamizi wa uchaguzi watawasaidia hakuna shida watapiga kura ".
"Serikali imeweka mipango mizuri na rafiki kwa makundi yote walemavu,wazee,wajawazito na inatia faraja kuwa haki ya Kila mmoja inatambulika na kuthaminika kutimiza haki ya kikatiba kuchagua kiongozi amtakae".Amesema Sixbeart mgombea
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupiga kura katika kituo cha Boma ,Kata ya Kimobwa, mji Kasulu mkoani Kigoma.Nao baadhi ya wananchi waliojitokeza kupiga kura wameeleza Hali ilivyo wakikiri uwepo wa amani na kuwashukuru wasimamizi wa uchaguzi ndani ya wilaya hiyo.
"Nawaasa wananchi wenzangu wasikubali kuyumbishwa na uvumi wa maneno ya watu kuhusu usalama bali wajitokeze kutimiza haki yao kikatiba ya kupiga kura na kuchagua viongozi wawatakao"amsema mmoja ya wananchi hao.
Mwandishi:Eunice Jacob
Mhariri:Harieth Dominick
0 Comments