Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanal Isaack Mwakisu leo amemkabidhi baiskeli Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Junga Wenslaus Lugaya almaarufu kama (Gadafi) ili kukamilisha lengo lake la kufika Ikilu ya Dodoma kwa kutumia baiskeli ikiwa ni katika hatua ya kutangaza Utalii na maendeleo yaliyopatikana katika mkoa wa Kigoma.
Zoezi hilo limefanyika katika viwanja vya ofisi ya Halmshauri mji Kasulu ambalo limehudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo na viongozi wa Serikali ili kumuaga Mwalimu Lugaya ambae pia ni mlezi wa Kasulu Jogging Club ya Kasulu mjini.
Kanali mwakisu, amefurahishwa na wazo la ubunifu wa Mwalimu huyo kuamua kutangaza maendeleo ya Mkoa wa Kigoma kwa kutumia njia hiyo kwani ni ubunifu wa hali ya juu na kuwataka watumishi wa sekta mbalimbali pamoja na vijana kuchangamkia fursa kwa kuwa wabunifu .
“Watu wengi hasa vijana wamekuwa wavivu wa kufikiri lakini ukiichangamsha akili yako kufikiria wazo la ubunifu ukija kwangu nitakuunga Mkono ili kutimiza lengo ambalo linaleta tija kwa jamii yetu,” amesema Kanal Mwakisu.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kasulu Mji Mwl. Vumilia Simbeye(kulia) akimkabidhi Bedera ya Kasulu Mji, Mwl.Wenseslaus Lugaya.
Safari ya Mwalimu Lugaya imeanza leo kuelekea mkoani kigoma ambapo kesho ataanza rasmi safari kutokea Mkoani Kigoma kuelekea jijini Dodoma kwa kupitia Tabora na Singida safari ambayo atasafiri kwa siku nane njiani.
Mhariri: Mussa Mkilanya.
0 Comments