Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Kigoma Mhe. Agripina Zaituni Buyogera amesifu wakazi wa Kijiji cha Nyangwa kata ya Makere kwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
"Kwakweli sikutegemea kuona vijana na wanawake wengi kujitokeza hivi hii ni ishara kubwa kuwa kundi hilo limepata muamko Mkubwa wa kupigania haki zao na hii ni kutokana na maendeleo yanayofanywa na serikali kuu" amesema mhe. Buyogela.
Mhe. Agripina Zaituni Buyogera akipokea maelekezo kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi kijiji cha Nyangwa.
Aidha Mhe. Buyogera amesema kupiga kura ni haki ya msingi ya kila Mtanzania mwenye sifa, hivyo wananachi wajitokeze wachague viongozi watakaoleta maendeleo."Katika Tanzania hii unapoona maendeleo makubwa ya miundombinu, elimu, Afya na maji nikwasababu ya kuwepo viongizi makini na wenye uchu wa maendeleo, hivyo wapigakura wasiangalie undugu wala urafiki bali wazingatie Kiongozi Bora," amesema mhe. Buyogela.
Jumla ya watanzania takriban milioni 31 wamesajiliwa
kupiga kura kwenye vijiji na vitongoji zaidi ya 75,000 nchini Tanzania Ili
kuchagua wawakilishi wa mitaa kwa muda wa miaka mitano ijayo.
Mwandishi:Mussa Mkilanya
Mhariri:Harieth Dominick.
0 Comments