Mbunge wa Kasulu Mjini Prof Joyce Ndalichako ameshiriki zoezi la Kupiga kura katika kituo cha Nyachijima kata ya Mrusi Halmashauri ya Mji Kasulu na kuwapongeza Wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la upigaji Kura.
Akizungumza na Buha Fm, mara baada ya kupiga kura leo, Prof. Ndalichako amewataka wapiga kura kufuata maelekezo ya wasimamizi wa uchaguzi ili kurahisisha zoezi hilo kutokana na watu kujitokeza kwa wingi katika kituo hicho
"Kama unavyoona foleni ni kubwa watu wamejitokeza kwa wingi naomba wasimamizi wajitahidi kuandisha haraka kidogo la sivyo watu watakakaa hapa muda mrefu”Amesema Prof.Ndalichako.
Katika hatua nyingine baadhi ya wananchi wa Halmashauri ya Mji kasulu wakizungumza na Buha Fm nyakati tofauti wamelalamikia zoezi hilo kwenda taratibu hivyo kusababisha kuchukua muda mrefu katika vituo vya kupigia kura.
Zoezi la Uchaguzi wa serikali za mitaa linaratibiwa na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa chini ya Ofisi ya Rais.
Mwandishi: Sharifat Shinji
Mhariri: Harieth Dominick
0 Comments