Aliyekuwa waziri wa usalama wa ndani nchini Kenya Profesa Kithure Kindiki ameapishwa rasmi kuwa naibu rais mpya wa Kenya,Kithure Kindiki anachukua nafasi ya Rigathi Gachagua aliyeondolewa madarakani.
Kindiki anachukuwa wadhifa huo baada ya siku kadhaa za makabiliano ya mahakama kati ya mawakili wa aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua na wale wa serikali ambae alienda mahakamani kuzuia kuapishwa kwa Kindiki baada ya kudai kwamba aliondolewa madarakani kinyume na sheria.
"Inaarifiwa katika taarifa ya umma kwamba hafla ya kuapishwa kwa Naibu Rais mteule itafanyika Ijumaa, Novemba 1, 2024, katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Kenyatta (KICC) katika kaunti ya Jiji la Nairobi, kuanzia saa 10 asubuhi" lilisema taarifa ya gazeti la serikali iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mawaziri Mercy Wanjau.
kushoto ni Naibu Rais wa Kenya Profesa Kithure Kindiki na kulia ni Rais Wiliam Ruto
Awali Bunge la Seneti nchini Kenya lilimepiga kura kwa kauli moja kumvua madaraka Naibu wa Rais Rigathi Gachagua Maseneta waliendelea kujadili hoja ya kumuondoa mamlakani huku Walipigia kura hoja zote 11 zilizowasilishwa dhidi ya Bw. Gachagua na hatimaye kuidhinisha hoja tano kati ya hizo.
Hafla ya kuapishwa imefanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (KICC) jijini Nairobi Nchini Kenya.
Mwandishi;Ellukagha kyusa
muhariri ; Ramadhan Zaidy
0 Comments