Rais Dkt. Mwinyi, Zanzibar ina mazingira rafiki uwekezaji.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amefungua rasmi ofisi ya wakala wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) iliyopo maeneo ya Minhang, jengo la Ling Hang Group, Shanghai tarehe 6 Novemba 2024.

Katika hafla hiyo fupi ya ufunguzi rasmi wa ofisi, Rais Dk. Mwinyi, amesema kuwa Zanzibar bado inahitaji wawekezaji katika sekta mbalimbali ili kuimarisha na kukuza uchumi wake.

 Amesisitiza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Aidha Rais Dk.Mwinyi ameongeza kuwa Serikali ya Zanzibar imedhamiria kuchochea ukuaji wa sekta ya utalii, kilimo, uvuvi, na viwanda ili kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi.

Kufunguliwa kwa ofisi hiyo ni hatua muhimu ya kufanikisha malengo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hususan kuvutia uwekezaji na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara baina ya Zanzibar na mataifa mengine.

Muhariri:Eunice Jacob.

Post a Comment

0 Comments