Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr Samia Suluhu Hasan ametaka Amani na utulivu kuendelea kudumishwa
katika kipindi chote cha zoezi la upigaji kura wa serikali za mitaa.
Rais Samia amesema hayo baadaya kupiga
kura katika kijiji cha Chamwino,Jijini Dodoma ambapo amesema zoezi la upigaji
kura ni utamaduni wa kawaida wa kidemokrasia hivyo hakuna sababu za mivurugano na
matokea yatolewe kama yatakavyoamuliwa na
wananchi.
Uchaguzi wa serikali za mitaa
unahusisha jumla ya Vijiji 12,333, Mitaa 4,269 na Vitongoji 64,274 nchi nzima.
Mwandishi: Harieth Dominick .
0 Comments