Rais Samia atoa maagizo mazito kufuatia kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Dar es salaam, Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Hospitali  ya Taifa Muhimbili na Idara ya Menejimenti ya maafa kufanya kila linalowezekana kufanikisha zoezi la uokoaji na Tiba kwa majeruhi.

Maagizo hayo ya rais yamekuja kufuatia kuanguka kwa jengo la ghorofa mbili lililopo Kariakoo Jijini Dar es salaam ambapo Mtu  mmoja amefariki dunai na wengine zaidi ya 28 wamejeruhiwa kufuatia kuanguka kwa jengo hilo ambapo tayari Serikali imeunda kamati ya uchunguzi kufuatia ajali hiyo iliyotokea leo asubuhi.

Jengo hilo ambalo lipo maeneo ya mtaa wa Kongo na Chikichi ambalo linatajwa kuwa ni la muda mrefu limeporomoka na kusababisha  kifusi cha jengo hilo kufunika baadhi ya maduka ya chini .



Kufuatia ajali hiyo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefika katika eneo la tukio nakuzungumza na wananchi ambapo amesema  hadi muda wa mchana leo ni watu 28 wameokolewa na kukimbizwa hospitali ya muhimbili, Temeke na Mwananyamala huku mtu mmoja akifariki dunia .

Post a Comment

0 Comments