Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa familia na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaza kutokana na kifo cha Dk Faustine Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani
(WHO), Kanda ya Afrika.
“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Dk Faustine
Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa
Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, kilichotokea
usiku wa kuamkia leo Novemba 27, 2024.”
“Ninatoa salamu za pole kwa familia, Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk Tulia
Ackson, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, wananchi wa Kigamboni, ndugu, jamaa, marafiki
na Watanzania wote.” Ameandika Rais Samia.
Dk Ndugulile alikuwa Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya
Dunia Kanda ya Afrika (WHO) ambaye alipaswa kuanza
majukumu hayo mapya Februari 2025.
Mwandishi:Harieth Dominick .
0 Comments