Ile dhamira ya Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuufanya mkoa wa Kigoma kuwa kitovu cha Biashara na uchumi katika ukanda wa Magharibi ameendelea kuionesha kwa vitendo.
Ambapo Novemba 21,2024 wananchi wa Kigoma wakiongozwa na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Kamishina Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto ndugu Thobias Andengenye walishuhudia uongozi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kikiingia mkataba wa miaka miwili na kampuni ya 'China Jiangxi International and Technology Co. LTD' kwa ajili ya kuanza ujenzi wa chuo kikuu kampasi ya Kigoma.
Ujenzi huo unatarajia kufanyika eneo la Uwekezaji KISEZ lililipo Manispaa ya Kigoma Ujiji Ambapo Rais Dkt.Samia amefungua alitoa kiasi cha Shilingi Billion ishirini na sita (Tsh 26,088,071, 158.84/=) za Kitanzania zitakazotumika kukamilisha mradi huo.
Baada ya kukamilika mradi huo kwa Mwaka wa Kwanza chuo kitachukua Wanafunzi Mia tatu (300) huku uwezo wake halisi itakuwa ni kuchukua Wanafunzi Elfu tano Mia Sita sabini na tatu (5673).
Naye mkuu wa mkoa wa Kigoma ametoa wito kwa wakazi na wazazi wa kigoma kuogeza bidii ya kusomesha watoto wao hasa katika masomo ya sayansi ili waweze kupata sifa ya kusoma katika chuo hicho.
"Tunatoa mwito kwa wazazi,walezi na vijana Wanafunzi wakazi wa Kigoma kusoma kwa bidiii hususan masomo ya Sayansi ili waweza kupata sifa stahiki za kusoma katika chuo hicho na wawe sehemu ya wanufaika wa fursa hiyo adhimu iliyotokana na maono ya Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan". amesema Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye.
Nakuombeni tujipange kimkakati na wana Kigoma mlioko nje ya Kigoma huu ni wakati sahihi wa kuja kuwekeza ili kila mmoja aweza kunufaika ipasavyo katika maendeleo haya makubwa ndani ya mkoa wetu wa Kigoma.
kwa upaqnde mwingine wakandarasi wamekumbushwa kuzingatia na kufanyia kazi ombi na hoja ya Mbunge wa kigoma mjini Kilumbe Shaaban Ng'enda ya kuwapa fursa ya kazi za kawaida wakazi wa Kigoma wakati wote wa ujenzi wa mradi huo na kusema kuwa swala hilo ni muhimu kwani itasaidia wananchi kuona kuwa mradi huo ni wao.
Mhariri: Ramadhani Zaidy
0 Comments