Raisi wa Burundi ametoa msamaha kwa Wafungwa 5442 sawa na asilimia 41 za wafungwa wote, 

Akizinduwa kampeni hio ya msamaha kwa wafungwa iliofanyika Mkoani  Muramvya leo  Raisi NDAYISHIMIYE amewataka waliofaidi na msamaha huo kuwa mfano bora kwenye jamii wasirudie tena vitendo vitakavyosababisha Kurudishwa Gerezani.

Katika hotuba yake Rais Evariste Ndayishimiye amesema amechukua hatua hiyo ili kupunguza matumizi ya serikali kutokana kutumia takribani franga bilioni 15 kugharamia shughuli za magereza kila mwaka.

wafungwa wakifuatilia  hotuba yake Rais Evariste Ndayishimiye ialiyoitoa mkoani Muramvya nchini humo. 

Asasi za kiraia zimetangaza kuridhishwa na kitendo hicho na kuomba kwamba kipindi cha wiki moja kilichotolewa na Raisi ili wafungwa hao waweze kuwa wameachiliwa huru

 Utafiti uliotolewa na shirika la kitaifa la kutetea haki za binadamu la CNIDH mwaka 2023, unaonyesha kuwa zaidi ya wafungwa elfu 13 walifungwa katika magereza tofauti nchini Burundi.

Mwandishi:David NDEREYIMANA

 Mhariri:Harieth Dominick

 

Post a Comment

0 Comments