Mkoa wa Kigoma umeandikisha wanafunzi 12,517 nje ya
mfumo wa rasmi elimu, na kurejesha shuleni wanafunzi 2,357 kwa mwaka 2023/2024.
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishina Jenerali mstaafu wa
Jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye, amesema hayo wakati akitoa
tathimini ya hali ya elimu kwa watoto wenye umri wa miaka 7- 15 mkoani humo.
Aidha amesema lengo la mkoa kwa mwaka 2025 ni
kuandikisha watoto 5,632 na kuwarejesha shuleni watoto 2001 waliokatisha masomo
kwa sababu mbalimbli .
"Katika tafiti inaonyesha kunawanafunzi wanakatisha masomo kwa hofu ya adhabu wanayopatiwa mashuleni pale wanapo kumbana na walimu wenye kutoa adhabu za maumivu na kushindwa kuhudhuria masomo yao na wengine kuwamua kuwacha shule kabisa".
Moja ya binti aliyekatisha masomo akizungumza na Buha
fm radio amesema alikatisha masomo baada ya kupata ujauzito tokana na kukosa
elimu ya makuzi kutoka kwa wazazi wake.
"Wanaacha pale ambapo amekosa alama nzuri za kumfanya kusonga mbele kutoka kidato cha pili kwenda kidato cha tatu nakuhisi kuwa akirudia darasa wale aliyosoma nao watamcheka na kumdhihaki nkumuona kama hana akili".
Aidha wamedai kuwa baadhi ya wazazi wanachangia watoto kuwa na mahudhurio hafifu na wengine kuacha shule kwani wamekuwa wakiwapa majukumu ya kwenda shamba na kukosa masomo.
Jumatano Novemba 24 ,2021 Aliyeku waziri wa elimu
sayansi na teknolojia Profesa Joyce Ndalichako alitangaza na kutoa walaka wa
serikali kuwaruhusu wanafunzi waliokatisha masomo kutokana na sababu mbali
mbali kurejea shuleni kwa mfumo rasmi .
Hilo
likaruhusu wanafunzi wote wenye nia ya kusoma hata waliopata ujauzito kurejea
shuleni baada ya kujifungua
ili kutimiza ndoto zao .
0 Comments