SADC kujadili mgogoro wa kisiasa Msumbiji.


Viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC wanatarajiwa kukutana  katika mji mkuu wa Zimbabwe Harare, kuujadili mzozo wa Msumbiji. 

Hayo yamejiri baada ya Mzozo wa kisiasa na kijamii unaozidi kuongezeka Msumbiji huku wakiufanya kuwa ajenda kuu ya mkutano wa kilele wa SADC ulioitishwa baada ya matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 9 kusababisha maandamano ya wiki kadhaa na kumfanya mgombea wa upinzani aliyeshindwa kupinga matokeo.

Kwa mjibu wa DW Watu wasiopungua 30 wanaripotiwa kuuawa katika maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi kufuatia ushindi wa mgombea wa chama tawala cha FRELIMO Daniel Chapo.

Katika hatua nyingine kiongozi wa upinzani Venancio Mondlane anayapinga matokeo hayo ambayo anadai kuwa yamechakachuliwa na kuitisha maandamano ya nchi nzima.

Siku chahce nyuma BBC iliripoti kuwa vyama vya upinzani vilidai kuwepo kwa udanganyifu mkubwa katika uchaguzi huku madai yao yanazingatiwa na Baraza la Katiba la Msumbiji ambalo linatazamiwa kutoa matokeo yake ya mwisho mwishoni mwa mwezi huu.

Ifahamike kuwa mkutano huo utajumuisha mataifa 16 nayozijumuisha Angola, Botswana, Visiwa vya Comoros, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Eswatini, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Ushelisheli, Tanzania, Zambia na  Zimbabwe, suala kuu katika agenda litakuwa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Msumbiji.

Mhariri; Sharifat Shinji

Post a Comment

0 Comments