Spika akerwa na utoro wa mawaziri Bungeni

 

Spika  wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson ameeleza kusikitishwa kwake na kitendo cha baadhi ya mawaziri kuendelea na tabia ya  kutohudhuria vikao vya bunge ili kujibu hoja za wabunge.

Amesema hayo  Novemba 1, 2024 bungeni jijini Dodoma na kusema kuwa hoja ya mawaziri kutohudhuria vikao vya bunge ni jambo ambalo limezungumzwa mara kadhaa bungeni lakini hakuna utekelezaji.

"Ilikuwepo hoja ya kuhusu mahudhurio ya mawaziri katika vikao vya bunge ni jambo ambalo nadhani tumelizungumza mara kadhaa hapa bungeni lakini naona sasa kuna changamoto wakati mwingine vikao vinaitiswa na serikali muda wa bunge, mwengine anafanya vikao kwa njia ya mtandao wakati yuko Dodoma"Amesema Dkt Tulia.

Aidha Dkt Tulia ameongeza kwa kusema kuwa hapo awali Rais Samia alitoa maagizo kuwa kipindi cha bunge mawaziri na manaibu waziri wote wawepo bungeni.

"rais samia aliangiza katika kipindi cha bunge mawaziri na manaibu wao wawe Bungeni, ambavyo wanakuwa hawapo sote tunajua hakuna kwa kupokea ushauri na mapendekezo ya bunge" ameongeza Dkt Tulia

Kwa mujibu wa spika wa bunge Tulia Ackson amesema kuwa ni vyema serikali kuwepo katika  vikao vya bunge ili kujibu hoja za wananchi kupitia wabunge wao.

Mwandishi; Ramadhan Zaidy

Post a Comment

0 Comments