Timu ya Manchester United imemtangaza RUBEN AMORIM mwenye umri
wa miaka 39 kuwa kocha mpya baada ya ERIK TEN HAG kuondoshwa katika timu hiyo
yenye masikani yake katika jiji la Manchester nchini Uingereza.
Ruben Amorim amesaini kandarasi ya mioaka miwili hadi mwaka 2027
akitoke Sporting Lisbon ya nchini Ureno huku akitarajiwa kuanza majukumu yake
Novemba 11 mwaka huu.
Mreno huyo amewahi kushindashinda mataji mawili ya ligi kuu ya Ureno, Primeira Liga akiwa na Sporting Lisbon, Manchester United imemuelezea Amorim kuwa ni moja wa makocha chipukizi na wenye kusisimua katika soka la ulaya.
RUUD VAN NISTELROOY ataendelea kushika usukani wa timu hadi Amorim atakapowasili Old Trafford wakati wa kipindi cha mapumziko ya ligi mwezi Novemba. Mechi ya kwanza ya Amorim itakuwa dhidi ya Ipswich Novemba 24.
United ilimtimua TEN HAG Jumatatu ya wiki hii baada ya kuwa na
mwendelezo mbaya wa matokeo katika ligi ya Uingereza ambampo anashika nafasi ya
14 akiwa ameshinda michezo michezo mitatu kati ya nane ya mwisho Amorim ni
kocha wa tano kujiunga na Manchester United tangu Sir Alex Ferguson alipoondoka
mwaka wa 2013.
Mhariri; Sharifa Shinji
0 Comments