Treni ya kisasa kuanza safari zake rasmi

 


Shirika la Reli Tanzania (TRC), leo Novemba 1, 2024 limeanzisha rasmi safari ya Treni ya umeme ya Mchongoko kutoka Mkoa wa Dar es salaam hadi Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza wakati wa kuanza kwa safari hizo jijini Da es salaam, Mkurugenzi wa shirika hilo Masanja Kadogosa amesema safari hizo zitasaidia kwa kiwango kikubwa katika kuchochea shughuli za maendeleo na uchumi kwani muitikio wa watanzania katika kutumia usafiri wa Treni ni mkubwa .

Masanja ameongeza kuwa kwa sasa shirika hilo linasafirisha watu kati ya elfu tisa hadi elfu kumi, huku idadi kubwa ya abiria inatarajiwa kuongezeka kutokana na  kuongezeka kwa safari za treni.

Abiria wa treni ya kisasa yenye kichwa cha Mchongoko

Kwa upande wa
ke mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema wamepokea abiria 320 waliowasili katika  stesheni ya Samia mkoani humo kwa kutumia Usafiri wa Treni ya kisasa iliyoanza safari yake kutoka Dae es Salaam kwa kutumia muda wa saa tatu

Aidha kwa mujibu wa Masanja amesema Treni hiyo imezingatia mahitaji yote ya abiria hasa ya watu wenye mahitaji maalumu, kwa kuwa na mazingira rafiki yanayozingatiamahitaji ya abiria wote.

mwandishi: Mussa Mkilanya

Muhariri; Ramadhani Zaidy

Post a Comment

0 Comments