Trump amemteua Mike Waltz kuwa mshauri wa Usalama wa Taifa


Saa 4 zilizopit


Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua Mike Waltz kuwa mshauri wake wa masuala ya Usalama wa Taifa, vyanzo viwili vinavyolifahamu suala hilo vimeliambia shirika la habari la Reuters siku ya Jumatatu.

Waltz, mfuasi kindakindaki wa Trump amekuwa mkosoaji mkubwa wa shughuli za China katika Ukanda wa Asia-Pasifiki na kuitahadharisha Marekani kujiandaa na mzozo mkubwa unaoweza kutokea kwenye ukanda huo.

Mwanajeshi huyo wa zamani amekuwa akizisifu sera za kigeni na mitizamo ya Trump huku akiikosoa vikali serikali ya Biden kwa namna ilivyowaondoa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan mwaka 2021.

Ushauri wa masuala ya usalama ni jukumu zito lisilohitaji kuidhinishwa na Seneti na Waltz atakuwa na jukumu la kumuarifu Trump masuala muhimu ya usalama wa taifa.

Trump aidha amemteua Seneta Marco Rubio kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Gazeti la New York Times limearifu.

haya yanajili mara baada ya  Rais huyo wa taifa kubwa lenye upinzani mkubwa na ukomavu wa  siasa na kupelekea Tramp kupita katika uchaguzi uliofanyika tarehe 5 november 2024 mwaka huu na Tramp kutangazwa mshindi  dhidi ya mpinzani wake kamala harris

Mwandishi: Abel  Mahenge 

Mhriri : Ellukagha  Kyusa 

Post a Comment

0 Comments