Urusi kutumia wanajeshi wa Korea Kaskazini.


 Takriban wanajeshi 11,000 wa Korea Kaskazini tayari wamewasili katika eneo la mpaka wa Urusi la Kursk. Haya yamesemwa jana na Ukraine huku kukiwa na hofu kwamba huenda wakatumiwa katika vita nchini Ukraine.

Katika hotuba yake ya kila jioni kwa njia ya vidio jana Jumatatu, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, alisema kuwa wanaona ongezeko la idadi ya wanajeshi wa Korea Kaskazini, lakini hawaoni kuongezeka kwa msaada wa silaha kutoka kwa washirika wao.

Zelensky amesema taarifa hiyo inatokana na uchunguzi wa idara ya kijasusi ya nchi hiyo.

Haijabainika ikiwa wanajeshi wa Pyongyang watapigana Ukraine

Ukraine inadhani kuwa hivi karibuni, wanajeshi wa Korea Kaskazini watatumwa naUrusi dhidi yake, ingawa wanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa pia wamesema wanajeshi hao wanaweza kupelekwa nchini humo labda kutekeleza majukumu ya mipangilio.

Mwandishi: Eunice Jacob.

Muhariri: Ellukagha Kyusa.


Post a Comment

0 Comments