Mkoa wa kigoma umetajwa kuwa ni miongoni mwa mikoa yenye idadi ndogo ya watu walioomba ajira katika kada ya Afya.
Naibu waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu leo ameonesha kushangazwa na jambo hilo
huku akitaja sababu kuwa ni kukwepa maeneo ya vijijini.
Amesema hatua hiyo ni matokeo ya Sekretarieti ya ajira
katika utumishi wa umma kuweka utaratibu wa kuomba ajira katika mikoa husika
kulingana na uhitaji.
Sekretarieti ya ajira kwa mwaka huu mwezi Juni ilitangaza
nafasi za kazi 9,483 katika kada ya Afya ambapo kila muombaji alilazimika
kuomba ajira katika mkoa ambao atafanya kazi.
Mhe. Sangu ametoa mfano katika Mkoa wa Kigoma kuwa
watumishi kada ya Afya wanaohitajika ni 400 lakini maombi yaliyopokelewa ni 200
pekee.
Mikoa ya Lindi, Mtwara na Katavi nayo ni miongoni mwa
mikoa yenye idadi ndogo ya maombi ya ajira katika kada hiyo, ukilinganisha na
uhitaji wakati Mikoa ya Dar es salaam, Mwanza na Dodoma ikiwa na idadi kubwa ya
waombaji.
Mwandishi: Mussa Mkilanya
0 Comments