Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe: Kanal Isaac Mwakisu leo ametoa wito kwa wananchi wa Kasulu kujitokeza kwenye vituo vyao walivyojiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kesho.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake amesema vituo vya kupiga kura vitafunguliwa saa mbili kamili asubuhi
na vitafungwa saa kumi kamili jioni.
"Wananchi mjitokeze kwa wingi katika vituo mlivyojiandikisha Ili kutimiza haki yenu ya kikatiba kuchagua kiongozi atakaeleta maendeleo ndani ya kata,mitaa, na vijiji." Amesema kanal Mwakisu.
Aidha Kanal Mwakisu amewahakikishia usalama wananchi kwenye vituo vya kupigia kura na kuongeza kuwa wananchi wanapaswa kuepuka kuvaa nguo zinazoashiria sare ya Chama chochote Cha kisiasa.
"kitu cha muhimu nawahakikishia wananchi wa kasulu kuwa kama serikali tumejizatiti kuimarisha ulinzi hivyo waondoe wasiwasi juu ya hilo tunatarajia idadi kubwa ya wananchi kujitokeza na kupiga kura" ameongeza Kanal Mwakisu.
wananchi wasikubali kuyumbishwa na uvumi wa maneno ya watu kuhusu usalama Bali wajitokeze kutimiza haki Yao kikatiba ya kupiga kura na kuchagua kiongozi amtakae.
Uchaguzi wa serikali za Mitaa utafanyika kesho Nov 27,2024 nchi nzima yenye kauli mbiu isemayo serikali za Mitaa sauti ya wananchi jitokeze kushiriki uchaguzi.
Mwandishi:Eunice Jacob.
Muhariri : Mussa Mkilanya.
0 Comments