Takriban watu 30 wanahofiwa kufariki dunia baada ya maporomoko ya ardhi yaliyosababisha na Mvua kubwa iliyonyesha Wilayani Bulambuli, mashariki mwa Uganda, siku ya Alhamisi, Novemba 28 mwaka huu.
Kaya 40 zinatajwa kufunikwa na nyingine kuharibiwa kabisa huku miundo mbinu kama barabara na madaraja kuharibiwa hali inayofanya kazi ya uokozi kuwa ngumu kwa vyombo vya uokozi.
Polisi nchini humo imesema watu zaidi ya 100 bado hawajapatikana ambapo mvua kubwa zilianza kunyenya tangu mwezi Octoba mwaka huu na sababisha Mavuriko katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
Nchi hiyo ya Afrika Mashariki imekumbwa na mafuriko na mvua kubwa katika siku chache zilizopita, huku serikali ikitoa tahadhari ya maafa baada ya ripoti za mafuriko na maporomoko ya ardhi.
Picha kwenye vyombo vya habari vya ndani zilionyesha maporomoko makubwa huku wanafamilia wakiomboleza, na wengine kuelezea masikitiko yao.
"Tulipoteza takriban watu 30," mkuu wa wilaya Faheera Mpalanyi aliambia AFP. Aliongeza kuwa miili sita, ikiwa ni pamoja na wa mtoto, imepatikana hadi sasa.
Mwandishi: Harieth Doinick
0 Comments