JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa
wawili ambao ni Ramadhan Tembo Mwakilasa (28) na Mariamu Charles Mwashambwa (28) Wakazi wa Jiji la Mbeya kwa tuhuma
za mauaji ya mtoto Chloy Ramadhan [04] kwa kumpiga fimbo sehemu mbalimbali za mwili.
Tukio hilo limetokea Novemba 25, 2024 saa 2:00 usiku Mtaa wa
TEKU viwandani , ambapo mtoto huyo alifariki dunia baada ya kupigwa fimbo
sehemu mbalimbali za mwili wake na baba yake mzazi Ramadhan
Mwakilasa akishirikiana na mama
yake wa kambo aitwaye Mariamu Charles Mwashambwa (28).
Uchunguzi umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni ukatili na
unyanyasaji wa kumuadhibu mtoto huyo baada ya kujisaidia kwenye nguo alizokuwa
amezivaa.
Jeshi la Polisi limewataka wazazi/walezi kuacha vitendo vya
ukatili kwa watoto vinavyokatisha maisha
yao kwa kisingizio cha makosa
badala yake watumie njia sahihi
za kurekebisha zisizo na madhara kwa
watoto.
Mwandishi:Harieth Doinick
0 Comments