Wenyeviti 108 na wajumbe 540 wa serikali ya mitaa katika Halmashauri ya Kasulu Mji Mkoani Kigoma leo wameapishwa tayari kuanza kutekeleza majukumu yao katika serikali za mitaa.
Akizungumza baada ya viongozi hao kula kiapo, Afisa uchaguzi Halmashauri ya Kasulu Mji Bw, Daniel Kaloza amewaasa viongozi hao kusimamia Sheria kanuni na kutimiza ahadi walizo toa kwa wananchi wakati wa Kampeni.
"sitegemei kuona kiongozi atakae hitaji rushwa ili kutatua changamoto na kero za wananchi wao kwani kufanya hivyo ni kinyume na kiapo cha uadilifu walichokiri wenyewe" Amesema Bw,Daniel Kaloza.
Salha Mangu na Thobias ni miongoni mwa wenyeviti waliokiri kiapo Cha uadilifu wamesema kuwa wapo tayari kiwatumikia wananchi bila kuangalia itikadi za vyama vya kisiasa.
"Tunashuru kwa wananchi kutuamini nakutupatia nafasi ya kuwa mwakilishi kwao na ahidi kufanya kazi kwa weledi kushirikiana kwa pamoja kutatua changamoto zinazo wakabili"Amesema Salha na Thobias.
Kwa upande wa Wajumbe Godfrey Buyagiro amesema kuwa amejipanga kufanya kazi kwa ukaribu na wananchi kutatua changamoto kwa kushirikiana na viongozi wa ngazi mbalimbali ndani ya kata na wilaya.
"tutakaa vikao na wananchi wetu kubaini changamoto kwa kushirikiana na diwani ambae ndiye mwenyekiti wa maendeleo wa kata lakini pia wananchi kushirikiana nasisi ili kuwa rahisi kwetu viongozi kupata utatuzi wa haraka" Amesema Godfrey Buyagiro.
Uchaguzi wa serikali za Mitaa ulifanyika Nov. 27 mwaka huu nchi nzima, ambapo wilaya ya Kasulu Mji ina mitaa 108, wenyeviti waliogombea ni 257 waliopita 108 huku CCM wakishinda viti 104,CHADEMA 3, ACT WAZALENDO kiti 1,
Upande wa Wajumbe kundi mchanganiyiko wagombea walikuwa 324 CCM viti 306,katika Wajumbe wanawake wagombea walikuwa 216 CCM wakishinda 211, viti 5 vikienda kwa vyama vingine vya siasa.
Mwandishi: Eunice Jacob
Mhariri: Harieth Dominick
0 Comments